Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Ikiwa ni katika muendelezo wa mauaji ya raia yanayofanywa na utawala haramu wa Israel, ndege za kivita za utawala huo hivi karibuni zilishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi ya Jabalia iliyoko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kuua kwa umati zaidi ya raia mia moja wa Palestina na kujeruhi wengine zaidi ya mia tatu.
Habari ID: 3477833 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/03
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Akizungumza leo katika sala ya Ijumaa ya mjini Tehran, Hujjatul Islam wal Muslimeen Kazem Sediqi amesema kuwa leo mrengo wa mapambano ya Kiislamu ni mrengo wa kimataifa na kuongeza kwamba mrengo huo umabadilisha dunia.
Habari ID: 3477832 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/03
Kadhia ya Palestina
DOHA (IQNA) - Muungano wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) ulitoa fatwa siku ya Jumanne, ukizitaka nchi za Kiislamu kuingilia kati ili kuwaokoa watu wa Gaza kutokana na mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477825 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/01
Jinai za Israel
TEHRAN (IQNA)- Wapalestina wasiopungua 400, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, wamethibitishwa kuuawa na kujeruhiwa baada ya mashambulizi ya anga ya utawala katili wa Israel dhidi ya wakimbizi ya Jabaliya katika Ukanda wa Ghaza.
Habari ID: 3477823 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/11/01
Kadhia ya Palestina
LONDON (IQNA) - Wazayuni hawawakilishi Uyahudi na wanataka "kuwaangamiza" watu wa Palestina, kuhani mwenye makao yake nchini Uingereza anasema huku kukiwa na mashambulizi ya Utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza yakiwa yamesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 7,000 wengi wakiwa ni wanawake, watoto na wazee.
Habari ID: 3477793 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/27
Taarifa Muhimu
TEHRAN (IQNA) –Wahadhiri 9,200 wa vyuo vikuu vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamelaani vikali ukatili wa utawala dhalimu wa Israel katika eneo la Palestina lililozingirwa la Ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3477783 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/24
AL-QUDS (IQNA) - Israel ilizuia makumi ya maelfu ya Wapalestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa siku ya Ijumaa ya 2 mfululizo.
Habari ID: 3477775 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/10/22
Milad un Nabii
AL-QUDS (IQNA) - Wapalestina waliadhimisha Maulidi yaani kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) huko Al-Khalil na hasa katikak Msikiti Ibrahim huku kukiwa na vikwazo vikali vilivyowekwa na utawala haramu wa Israel ambao unaongoza kampeni ya kupinga Maulidi.
Habari ID: 3477668 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/29
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Vikosi vya utawala katili wa Israel siku ya Jumatano viliwashambulia Wapalestina, wakiwemo wanawake na watoto, ambao walikuwa wakiadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) huko Al Quds (Jerusalem) Mashariki. Mji huo mtakatifu unakaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477664 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/28
Watetezi wa Quds Tukufu
TEHRAN (IQNA)- Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Mauritania wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott, wakilaani kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Waarabu na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3477643 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/23
Kadhia ya Palestina
AL-QUDS (IQNA) - Msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa al-Quds (Jerusalem) ni mahali pa ibada kwa Waislamu peke yao na ni haki takatifu isiyopingika kwao, mkuu wa Kamati ya Juu ya Rais ya Masuala ya Kanisa huko Palestina alisema.
Habari ID: 3477628 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/20
Ukombozi wa Palestina
TEHRAN (IQNA) Harakati ya Mapambano (Muqawama) ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imekosoa vikali kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ya kuyataka mapambano ya wapigania ukombozi Wapalestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kuwa eti ni "vurugu" na kusisitiza kwamba kinachofanyika katika ardhi za Palestina ni haki ya kujihami dhidi ya utawala unaokalia ardhi kwa mabavu.
Habari ID: 3477602 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/15
Mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya)
TEHRAN (IQNA)- Viongozi wa harakati za mapambano ya Kiislamu (Al-Muqawama Al-Islamiya) za Palestina na Lebanon wameapa kushirikiana ili kutoa jibu la pamoja dhidi ya sera za uvamizi za utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3477543 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/03
Kadhia ya Palestina
Al QUDS (IQNA) - Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya Ijumaa ya jana iliyosaliwa kwenye Msikiti wa Al-Aqsa mjini Al Quds (Jerusalem) licha ya kuwekewa vizuizi na kukabiliwa na hatua kali za kiusalama zilizochukuliwa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel katika mji huo unaoukalia kwa mabavu.
Habari ID: 3477538 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/02
Kadhia ya Palestina
TEHRAN (IQNA)- Baada ya maandamano makubwa ya wananchi wa Libya kulaani kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo na Waziri wa Mambo ya Nje wa utawala haramu wa Israel, Waziri Mkuu wa Libya amesema: Tripoli inaunga mkono suala la ukombozi wa Palestina.
Habari ID: 3477534 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/09/01
Watetezi wa Palestina
TUNIS (IQNA) - Rais wa Tunisia amesistiza kuwa nchi yake kati haitaanzisha uhusiano na utawala haramu wa Israel , akisema neno hilo halipo hata katika kamusi ya Tunisia.
Habari ID: 3477527 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/31
Mapambano dhidi ya Wazayuni
TEHRAN (IQNA)-Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Sayyid Hassan Nasrallah amewaonya viongozi wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kwamba mauaji yoyote yatakayofanywa ndani ya ardhi ya Lebanon ya kumlenga raia wa Lebanon, Palestina au Iran au raia wa nchi nyingineyo hayatapita bila ya jibu.
Habari ID: 3477514 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/29
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) - Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imeisitiza umuhimu wa kuhifadhi hadhi ya kihistoria na kisheria ya maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo huko al-Quds (Jerusalem).
Habari ID: 3477482 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/22
Diplomasia
ALGIERS (IQNA)- Naibu Spika wa Bunge la Algeria amesisitiza kuwa, taifa hilo la kaskazini mwa Afrika halitafuata mkumbo wa nchi nyingine za Kiarabu wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, akisisitiza kuwa Waalgeria wanautazama utawala huo kuwa wa kikoloni.
Habari ID: 3477450 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/08/17
Jinai za Israel
AL-QUDS (IQNA) – Utawala haramu wa Israel unapanga kuteka maeneo ya kiakiolojia ya Wapalestina kote Ukingo wa Magharibi, Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) ilionya.
Habari ID: 3477292 Tarehe ya kuchapishwa : 2023/07/16