IQNA – Chuo cha Masomo ya Kiislamu cha Sarajevo kimeandaa tukio lake la kila mwaka la “Usiku na Qur’ani,” likiwakutanisha wanafunzi na wahifadhi wa Qur’ani kwa jioni ya usomaji, tafakuri na kuthamini Kitabu cha Mwenyezi Mungu.
IQNA – Qari maarufu wa Misri, Abdul Fattah Tarouti, ametoa wito wa kuepuka mifarakano miongoni mwa wahudumu wa Qur’ani Tukufu kufuatia mjadala ulioibuka kuhusu usomaji wa Qari mwenzake, Ahmed Ahmed Nuaina.
IQNA – Lengo la elimu ya Qur’ani linapaswa kwenda mbali zaidi ya kuhifadhi, kuelekea kuunda “watu wa mfano wa Qur’ani hai” wanaoathiri jamii kupitia mwenendo wao, asema Hujjatul-Islam Seyyed Mohammad-Mehdi Tabatabaei kutoka Iran.
IQNA – Mitihani ya awali imeanza rasmi kwa washiriki wa kimataifa wanaojiandaa kushiriki katika Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur’ani, yanayoandaliwa na Wizara ya Awqaf ya Misri, yaliyopangwa kufanyika mwezi Disemba 2025.
IQNA – Msingi wa jamii ni ushirikiano, kushirikiana, na kubadilishana manufaa. Kwa hivyo, mtazamo wa kielimu wa Kiislamu umechukulia ushirikiano kuwa miongoni mwa mahitaji ya fikra za kimaadili.
IQNA – Mwana wa qari mashuhuri wa Qur’ani kutoka Misri, Sheikh Abdul Basit Abdul Samad (rahimahullah), ambaye sauti yake imehifadhiwa katika nyoyo za Waislamu duniani kote, amefariki dunia mjini Cairo siku ya Ijumaa, tarehe 31 Oktoba 2025.
IQNA – Kuzungumzia suala la “ Kupokonya Silaha Harakati za Muqawama” si chochote ila ni ndoto ya kufikirika, kwani maana yake ni kuwavua watu utashi wao na utambulisho wao, amesema mchambuzi wa kisiasa wa Kipalestina.
IQNA – Kituo cha Maendeleo ya Elimu kwa Wanafunzi wa Kigeni katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kimetangaza uzinduzi wa matawi mawili mapya ya Shule ya Kuhifadhi na Kusoma Qur’ani ya Imam el-Tayeb.
IQNA – Akifafanua dhana ya Yawm At-Taghābun, mwanazuoni wa chuo kikuu cha kidini kutoka (Hawzah) Iran amesema kuwa katika Siku ya Kiyama, mtu ataonyeshwa si tu matokeo ya matendo yake, bali pia mahali pake palipopotea Peponi—mandhari itakayokuwa majuto makubwa na mateso ya kiroho yasiyoelezeka.