Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Hivi karibuni Sheikh Shadhilii alifanya safari nchini Iraq na kuadhini katika Msikiti wa Kufa nchini humo, jambo lililosababisha afutiwe uwanachama wake kwenye muungano huo. Muhammad Mahmoud al Batlawi Mkuu wa Muungano wa Wasomaji wa Qurani Tukufu nchini Misri amesema kuwa, na hapa tunamnukuu: ' Kuna ulazima wa kuchukuliwa hatua za kuzungumza kwa kina na Dakta Ahmad al Tayyib Mkuu wa Chuo Kikuu cha al Azhar na Muhammad Mukhtar Waziri wa Waqf wa Misri yenye lengo la kuwapiga marufuku wasomaji wa Qurani Tukufu kufanya safari katika nchi za Iran na Iraq, ili lisijitokeza tena suala kama hili', mwisho wa kunukuu. Muhammad Mahmoud al Batlawi ameongeza kuwa, hii si mara ya kwanza kwa wasomaji Qurani Tukufu wa Kimisri kufanya safari katika nchi za Iran na Iraq na kuadhini kwenye misikiti mbalimbali ya nchi hizo.