Kwa mujibu wa gazeti la Al Masri Al Youm, Ubalozi wa Misri nchini Brazil umesema hotuba iliyorekodiwa ya Sheikh Tayyib ilirushwa hewani wakati wa sherehe za ufunguzi wa mashindano ya fainali za soka duniani nchini Brazil.
Sheikh Tayyib aliombwa rasmi na serikali ya Brazil kutoa hotuba katika ufunguzi wa Kombe la Dunia kuhusu wito wa Uislamu wa kuwepo amani katika maeneo mbali mbali mbali duniani.
Hotuba ya Sheikul Azhar iliashiria aya ya 13 ya Surat Hujuraat isemayo "Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari".
Sheikh Tayyib amesisitiza kuwa Uislamu unapinga machafuko, misimamo mikali na taasubi na kwamba dini hii tukufu inalipa umuhimu suala la kueneza utamaduni wa amani.
1416531