Hujjatul Islam Ali Reza Mirjalili, Mwambata wa Kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Brazil, aliiambia IQNA kwamba kozi hiyo inalenga kuongeza maarifa ya Qur'ani na kuimarisha ujuzi wa usomaji miongoni mwa Waislamu wa Brazil, huku pia ikifundisha walimu wa baadaye wa Qur'ani. "Mpango huu unalenga kuongeza uelewa wa Qur'ani miongoni mwa jamii ya Waislamu nchini Brazil na Amerika ya Kusini," Mirjalili alisema.
Kozi hiyo, itakayofanywa mtandaoni kwa vikao 12, itaanza Januari 1, 2025 kwa siku tatu.
Masharti ya usajili ni pamoja na kuwa na umri wa angalau miaka 15, kuwa na ujuzi wa kusoma Qur'ani, na kuonyesha uwezo wa kufundisha kanuni za Qur'ani.
Kozi hiyo itaongozwa na waalimu maarufu, wakiwemo Hujjatul Islam Ali Ghaseemi, mwalimu wa kimataifa wa Qur'ain na mkurugenzi wa Kituo cha Qur'ani na Hadith, na Hujjatul Islam Ali Reza Mirjalili, mwandishi na mwalimu wa kimataifa wa Qur'ani anayejua lugha kadhaa
Akitoa muktadha kuhusu Brazil, Mirjalili alielezea kuwa ni nchi kubwa na yenye idadi kubwa ya watu Amerika Kusini, ikiwa na zaidi ya wakazi milioni 220. Ingawa ni nchi yenye wafuasi wengi wa Katoliki, Brazil inaunga mkono uhuru wa dini na ina zaidi ya Waislamu milioni 10, wengi wao wakiwa na asili ya Kiarabu. Takriban asilimia 40 ya idadi ya Waislamu nchini Brazil wanajitambulisha kama Shia, na jamii ya Wairani inakadiriwa kuwa na watu chini ya 5,000, alisema.
3491278