IQNA

Jinai za Israel

Brazil: Utawala wa Israel lazima Ifuate amri ya ICJ huko Gaza

17:17 - February 27, 2024
Habari ID: 3478421
IQNA - Brazil imesisitiza haja ya utawala haramu wa Israel kufuata kikamilifu hatua za dharura zilizoamriwa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi uliopita kuhusu hali ya Ukanda wa Gaza.

"Brazil inaamini kuwa ni jukumu lake, lakini pia lile la baraza hili kupinga vikali aina yoyote ya ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia, chuki dhidi ya Wayahudi au Uislamu," Waziri wa Haki za Kibinadamu na Uraia wa Brazil Silvio Almeida aliambia Baraza la Haki za Kibinadamu huko Geneva siku ya Jumatatu, akilaani mashambulizi yanayoendelea huko Gaza.

Alibainisha kuwa nchi yake inalaani vita visivyo na mlingano na matumizi ya nguvu ya utawala haramu wa Israel ambao umesababisha vifo vya karibu watu 30,000 huko Gaza, aghalabu wakiwa ni wanawake na  watoto.

"Wengi wao wanawake na watoto, (Israel) iliwaondoa kwa nguvu zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Gaza na kuwaacha maelfu ya raia bila umeme, maji ya kunywa, chakula na misaada ya kimsingi ya kibinadamu," aliongeza Almeida.

Aliongeza kuwa Brazil inaona kuwa ni wajibu wa baraza hilo "kuheshimu kujitawala kwa watu" na kutafuta suluhu la amani kwa migogoro na kupinga aina zote za ukoloni mpya na ubaguzi wa rangi.

Akirejelea kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, iliyowasilishwa na Afrika Kusini mwezi uliopita, Almeida alitoa wito kwa Israel "kuzingatia kikamilifu hatua za dharura zilizoamriwa na mahakama kukomesha ukiukaji mkubwa wa haki za kibinadamu."

"Tunathibitisha kwamba uvamizi wa Israel katika ardhi ya Palestina ni kinyume cha sheria, na unakiuka viwango vya kimataifa," aliongeza.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Uamuzi wa muda wa mwezi Januari uliiamuru Israel kusitisha vitendo vya mauaji ya halaiki na kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba misaada ya kibinadamu inatolewa kwa raia huko Gaza. Hatahivyo utawala wa Kizayuni wa Israel, ukiwa unapata himaya kamili ya Marekani, umekaidi amri ya mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa na umeendeleza jinai ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina Gaza.

3487347

Habari zinazohusiana
captcha