IQNA

Rais Rouhani asema Iran italinda maeneo matakatifu Iraq

15:49 - June 19, 2014
Habari ID: 1420250
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema taifa la Waislamu la Iraq litafanikiwa kuwarudisha nyuma magaidi na waungaji mkono wao kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu na kwamba Jamhuri ya Kiislamu itafanya kila iwezalo kulinda maeneo matakatifu nchini Iraq.

Akizungumza katika mkoa wa Lorestan magharibi mwa Iran jana Jumatano, Rais Rouhani ameongeza kuwa madola yote makubwa, mamluki na magaidi wanapaswa kufahamu kuwa taifa adhimu la Iran litafanya kila liwezalo kulinda maeneo matakitifu katika miji ya Iraq ya Karbala, Najaf, Kadhimiyya na Samarra.

Rais Rouhani ameendelea kusema kuwa, idadi kubwa ya watu wa Iran wametangaza kuwa wako tayari kuelekea Iraq kulinda maeneo matakatifu ya Kiislamu na kukabiliana na magaidi. Ameongeza kuwa wananchi waliojitolea wa Iraq kutoka madhehebu ya Shia na Sunni na pia Wakurdi tayari wanakabiliana na magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh.

Tarehe 10 Juni kundi hilo linalojiita eti Dola la Kiislamu la Iraq na Sham lilichukua udhibiti wa makao makuu ya mkoa wa Nainawah, Mosul na maeneo ya karibu. Vikosi vya jeshi la Iraq vinaendeleza mapambano dhidi ya magaidi hao wa kitakfiri.

1419968

Kishikizo: iran iraq rouhani daesh
captcha