Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa, awali wanamgambo wa Daesh waliwafukuza wenyeji katika eneo hilo hadi umbali wa mita 500 na kisha kuanza kuliharibu kaburi la Nabii Yunus AS baada ya kuweka mada za milipuko. Kiongozi wa Idara ya Wakf katika mkoa wa Neinawah amesema kuwa, wanamgambo wa kitakfiri licha ya kubomoa kaburi la Nabii Yunus AS, wametekeleza jinai nyingine nyingi kwa kubomoa Misikiti kadhaa ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia na Suni katika mji wa Mosul, makao ya jimbo la Neinawah. Mashuhuda hao wameeleza kuwa, magaidi wa Daesh waliwazuia Waislamu kufanya ibada katika eneo hilo na kisha kuweka mada za milipuko ndani ya kaburi hilo la Mtume Allah.