IQNA

Jumatatu ni Idul Fitr katika baadhi ya nchi za Kiislamu

12:09 - July 28, 2014
Habari ID: 1434339
Baadhi ya Waislamu katika nchi za Iraq, Uturuki, Qatar, Misri, Saudi Arabia na Bahrain leo wanasherehekea sikukuu ya Idul Fitr baada ya kutangazwa rasmi mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani katika nchi hizo.

Taarifa zinasema kuwa, katika nchi nyingine kama vile Umoja wa Falme za Kiarabu, Jordan, Kuwait, Yemen, Syria, Lebanon, Afghanistan, Tajikistan, Kazakhstan na Palestina leo Jumatatu ni tarehe Mosi Shawwal. Hali kadhalika, baadhi ya Waislamu nchini Rwanda na Kenya leo wanasherehekea sikukuu ya Idul Fitr.
Hata hivyo, nchi nyingi duniani zimetangaza kuwa kesho Jumanne ni tarehe Mosi Shawwal. Nchi kama vile Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Algeria, Pakistan, Tanzania na Azerbaijan zimetangaza kuwa sherehe za Idul Fitr zitaanza kesho Jumanne.
1433605

captcha