IQNA

Imam Khamenei

Palestina ipewe kipaumbele katika Ulimwengu wa Kiislamu

19:51 - July 29, 2014
Habari ID: 1434649
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba, ulimwengu wa Kiislamu unapasa kuipatia kipaumbele kikubwa kadhia ya Ghaza.

Akiuhutubia umati mkubwa wa waumini walioshiriki kwenye ibada ya Sala ya Idul Fitr iliyosaliwa mapema leo asubuhi mjini Tehran, Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesisitiza kwamba, leo hii suala linalopasa kupewa kipaumbele zaidi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kadhia ya Ghaza, na kuongeza kwamba walimwengu wanapasa kuonyesha msimamo wao kuhusiana na kadhia hiyo.

Ayatullahil Udhma Khamenei ameongeza kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unafanya mauaji ya kimbari huko Ghaza na kusisitiza kwamba kinachoshuhudiwa huko Ghaza ni maafa makubwa zaidi ya kihistoria. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kwamba watenda jinai hizo na washirika wao wanapaswa kushitakiwa kwenye vyombo vya sheria vya kimataifa. Ayatullah Khamenei amevitaka vyombo vya habari duniani kupaza sauti zao na kuwafichua watenda jinai wa Kizayuni, iwe wale walioko ndani au nje ya uongozi au wale wanaousaidia utawala huo khabithi kwa namna moja au nyingine. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kuwa, nguvu za muqawama wa wananchi wanaokabiliwa na mzingiro huko Ghaza bado ziko imara na kusisitiza kwamba hatima ya mashambulio ya Wazayuni maghasibu, ni ushindi kwa wananchi wa Palestina.

Ayatullah Khamenei amebainisha kuwa, adui Mzayuni anajua wazi kwamba, atakabiliwa na hali mbaya zaidi iwapo ataamua kuendeleza mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina wa Ghaza. Kiongozi Muadhamu amesisitiza kwamba watenda jinai wote duniani wanashinikiza usitishwaji vita ili kuuokoa utawala wa Kizayuni wa Israel. Akielezea juhudi zinazofanywa na viongozi wa kisiasa wa madola ya kibeberu duniani za kutaka makundi ya Kipalestina ya Jihadul Islami na Hamas yapokonywe silaha, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, ulimwengu wa Kiislamu unapaswa kuwasaidia kisilaha kadri uwezavyo wananchi wa Palestina  ili waweze kupambana kikamilifu na majeshi ya utawala ghasibu wa Israel.

1434597

captcha