IQNA

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Isalmi ya Palestina

Israel ilipata pigo la kistratijia katika vita vya Ghaza

17:01 - September 09, 2014
Habari ID: 1448553
Ramadhan Abdullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema utawala wa Kizayuni wa Israel ulipata pigo la kistratijia hivi akribuni katika vita vyake vya siku 51 dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Kiongozi huyo wa Palestina ameyasema hayo katika hotuba yake kwa Kikao cha kwanza cha kimatiafa cha  'Maulamaa wa Kiislamu Wanaounga Mkono Harakati ya Muqawama' kinachofanyika Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika hotuba yake kwa njia ya video, alisema kuwa, 'Utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu ulipata pigo kubwa katika vita vya hivi karibuni huko Ghaza. Amesema utawala huo ghasibu ulipata pigo la kijasusi, kijeshi, kitratijia na kimaadili. Sambamba na kumshukuru Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na wapenda uhuru kote duniani ambao wametoa himaya yao kwa Wapalestina, Ramadhan Abdullah amesema , 'ushindi wa  Ghaza ni ushindi wa umma wote wa Kiislamu.'
Kongamano hilo la siku mbili limewaleta pamoja wasomi na maulamaa wa Kiislamu zaidi ya 200 kutoka nchi 53 kwa lengo la kuunda 'Jumuiya ya Maulamaa wa Muqawama.'

1448519

captcha