Khaled al Obeidi, ameeleza kuwa, idadi ya raia wa Kiarabu na wa kigeni imefikia milioni 4.5 kutoka nchi 60 tofauti duniani, wengi wao kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwamba hadi sasa Wairaq 13 milioni wameelekea kwenye mji huo.
Maafisa wa Iraq walitangaza wiki iliyopita kwamba, raia wa Iran zaidi ya milioni moja walivuka mpaka na kuingia nchini humo kwa azma ya kuelekea Karbala, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa.
Maombolezo ya siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala mnamo mwaka 61 Hijria. Mjukuu huyo wa Mtume na masahaba wake walipigana na jeshi la utawala dhalimu wa Yazid bin Muawiya uliokuwa umepotosha dini na mafundisho yake na wakauawa shahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.../mh