IQNA

Morocco kutoa mafunzo kwa Maimamu wa misikiti ya Ufaransa

16:54 - December 22, 2014
Habari ID: 2625018
Baada ya kutoa mafunzo kwa Maimamu wa miskiti kutoka nchi kadhaa za Afrika, Morocco sasa imesema itatoa mafunzo kwa maimamu 50 kutoka Ufaransa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mafunzo hayo yattahusu tafsiri ya Qur'ani Tukufu, Sira ya Mtume Muhammad SAW na pia masomo ya awali kuhusu teknolojia ya habari na mawasiliano.
Wahubiri hao wa Kiislamu wanatazamiwa kuhubiri Uislamu wenye mitazamo ya wastani sambamba na kupambana na mfunzo yenye misimamo mikali .
Hivi karibuni  Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq alisema kuwa magaidi 200 wa kundi la kitakfiri la Daesh (ISIS au ISIL) walikamatwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris. Adnan al Assadi ameeleza kuwa magaidi hao walitiwa mbaroni kutokana na ushirikiano kati ya Iraq na shirika la upelelezi la Ufaransa.
Takwimu mpya za hivi karibuni zinaonyesha kuwa Waingereza ndio raia wengi walio katika kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh kati ya nchi za Magharibi. Takwimu hizo mpya zinaonyesha kuwa, hadi sasa Waingereza wapatao elfu mbili wamejiunga na kundi la kigaidi la Daesh. Ripoti iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka huu na Umoja wa Mataifa ilionyesha kuwa, raia wa nchi za nje wasiopungua elfu 15 wameleekea Syria na Iraq kwa minajili ya kujiunga na Daesh na makundi mengi ya kigaidi.../mh

2624965

captcha