Imepokelewa kuwa Mtume Muhammad (SAW) amesema: “Ibada bora zaidi ni kuomba msamaha; kwa sababu hili ndilo neno la Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake aliposema:
‘Basi jueni kuwa hapana mungu ila Allah, na ombeni msamaha wa dhambi zenu.’” (Surah Muhammad, aya ya 19).
Aidha Hadithi nyingine inasema kuwa dua bora ya msamaha na ibada bora zaidi ni kutamka kauli tukufu: “La ilaha illa Allah.”
Katika Nahj al-Balagha, hekima ya 417, Imam Ali (AS) amesema: “Istighfar ni shafaa (tiba) yenye thamani kubwa, ni dua iliyo kamili zaidi, ni silaha yenye nguvu kwa wenye dhambi, na ni mkombozi bora kutoka katika madhambi.”
Imam Sadiq (AS) amesema: “Wakati Mwenyezi Mungu anapomkusudia kheri mja wake na akafanya dhambi, humuadhibu na kumkumbusha kuomba msamaha. Lakini akimkusudia shari na akafanya dhambi, humruzuku neema ili asahau kuomba msamaha na aendelee katika hali hiyo. Hii ndiyo maana ya maneno ya Mwenyezi Mungu: ‘Tunawaacha wale wanaokadhibisha aya zetu kwa hatua, hadi waangamie.’” (Surah Al-A‘raf, aya ya 182).
3495191