Kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa Mnara wa Milad pembizoni mwa Mashindano ya Tano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo Waislamu.
Kongamano hilo linatazamiwa kufunguliwa kwa hotuba ya Ayatullah Mohsen Araki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu. Kongamano hilo pia litahutubiwa na mwanazuoni wa Ufaransa na mtarjumu ya Qur’ani Yahya Bonnaud.
Kongamano hilo na mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Harakati za Qur’ani ya Wasomu wa Vyuo Vikuu vya Iran. Jumuiya hiyo ni kitengo cha Taasisi ya Jihadi ya Vyuo Vikuu kupitia Kituo cha Kikakademia cha Elimu, Utamaduni na Utafiti.../mh