Sayyid Hassan Nasrullah amesema kuwa, upande pekee usiohisi hatari ya kundi hilo la kigaidi, ni utawala wa Kizayuni wa Israel. Katibu Mkuu wa HIzbullah amelaani jinai ya kutisha ya kundi la Daesh ya kuwauwa Wakristo 21 wa Kimisri nchini Libya na kusisitiza kwamba kitendo hicho kisicho cha kibinadamu hakikubaliki hata kidogo. Sayyid Hassan Nasrullah amezungumzia pia hatua ya anayejiita Khalifa wa Daesh ya kumteua mtawala wa Makka na Madina na kusisitiza kwamba, lengo kuu la Daesh ni Makka na Madina na wala siyo Baitul Muqaddas, na viongozi wa Saudi Arabia wanapaswa kuwa macho na harakati hiyo. Katibu Mkuu wa Hizbullah amewataka Waislamu wote ulimwenguni kujifunga mkanda kwa lengo la kuilinda dini tukufu ya Kiislamu ambayo inachafuliwa na magaidi wa Daesh. Amesema kuwa, nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na zile za Magharibi zinazowaunga mkono magaidi wa Daesh zinapaswa kuelewa kwamba, umefikia ukomo kwa kundi hilo kulichezea jina la Uislamu.../MH