IQNA

Saudi Arabia inatekeleza jinai nchini Yemen

11:23 - April 15, 2015
Habari ID: 3148169
Afisa mwandamizi wa Harakati ya Hizbullah nchini Lebanon amelaani hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia nchini Yemen na kuitaja kuwa jinai huku akiuonya utawala huo kibaraka wa Marekani kuwa utapata hasara kubwa.

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassem alitoa matamshi hayo katika mahojiano na Shirika la Habari la Associated Press siku ya Jumatatu ambapo aliitaja serikali ya Marekani kuwa mshirika na mhusika katika hujuma na jinai za Saudia nchini Yemen. Amesisitiza kuwa  utawala huo wa kiimla katika Ghuba ya Uajemi umetekeleza  ‘kosa la kistratijia’ kwa kuivamia Yemen.
Sheikh Qassem amesema kuwa mgogoro wa sasa Yemen utaathiri eneo lote la Mashariki ya Kati na kuongeza kuwa Saudi Arabia itakumbwa na matatizo ya ndani kutokana na vita vya Yemen. Aidha Sheikh Qassem ameilaumu Saudi Arabia kwa kuunga mkono magaidi wenye mfungamano na al-Qaeda nchini Yemen.
Wakati huo huo Msemaji wa jeshi la Yemen, kamanda Sharaf Ghalib Luqman amesema kuwa, jibu la mashambulizi ya kichokozi ya Saudi Arabia na waitifaki wake dhidi ya watu na taifa la Yemen, yatatolewaa hivi karibuni na litakuwa kali mno. Luqman amesema kwamba, wahanga wakubwa wa mashambulizi ya Saudia ni raia wasio na hatia na kwamba hadi sasa watu 2051 wameuawa na wengine 3897 kujeruhiwa.../mh

3091584

captcha