Saudi Arabia wiki iliyopita ilitangaza kuwa imesitisha mashambulizi yake ya siku 27 huko Yemen baada ya kuuwa raia wasio na hatia wa Yemen zaidi ya elfu tatu wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kubomoa miundo mbinu ya nchi hiyo, hata hivyo masaa mawili baada ya kutangaza kusitisha hujuma zake za kijeshi katika nchi hiyo ya Kiarabu, ndege za utawala huo vamizi kwa mara nyingine tena zilianza kuyashambulia maeneo ya raia na kubomoa miundo mbinu ya Yemen.
Wakati huo huo habari kutoka Yemen zinarifu kuwa, makundi ya wanamapinduzi wa nchi hiyo wamewataka wananchi kufanya maandamano makubwa ya mshikamano hii leo kote nchini humo, ili kumpinga adui Saudi Arabia.../EM