Kikao hicho kilifunguliwa Jumanne kwa hotuba ya kwa kuhudhuriwa na Rais Macky Sall wa nchi hiyo. Iyad Madani, Katibu Mkuu Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu, Mkuu wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Utamaduni na Habari wa OIC na vile vile Mawaziri wa Utamaduni na Habari wa nchi za Kiislamu pia wamehudhuria na kuhutubi katika kikao hicho cha Dakar.
Semina hiyo ya siku mbili ilitupia jicho masuala mengi kama mazungumzo kati ya tamaduni na staarabu mbalimbali na pia nafasi ya vyombo vya habari vya Ulimwengu wa Kiislamu katika kuiunga mkono Quds Tukufu na kadhia ya Palestina.../EM