IQNA

Iran yataka Dunia izuie kuendelea hujuma ya kijeshi Yemen

18:33 - May 07, 2015
Habari ID: 3269138
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za kusitisha hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bi. Marzieh Afkham ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran katika mkutano wa kila wiki na waandishi habari na kuongeza kuwa: 'Hii leo Yemen inakaribia kukumbwa na maafa makubwa ya kibinadamu.' Ameelezea masikitiko yake kuwa nchi vamizi zimeizingira nchi hiyo na kuweka vizingiti na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia nchini humo. Afkham amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza mazungumzo na nchi kadhaa pamoja na jumuiya za kimataifa kwa lengo la kutatua matatizo ya Yemen sambamba na kufungua njia za kutumwa misaada ya kibinaadmau nchini humo. Amesema kuwawekea mzingiro watu wa Yemen ni jambo lisilokubalika na kwamba jinai hiyo itabakia katika kumbukumbu za mataifa ya bara Arabu.../mh

3261806

Kishikizo: iran yemen afkham saudi
captcha