Wameandamana wamelaani vikali mauaji ya umati ya Waislamu wasio na ulinzi wala hatia wa Yemen ambao wamepoteza maisha katika hujuma zinazoongozwa na utawala dhalimu wa Saudi Arabia. Aidha waandamanaji hao wametaka jinai hizo za Saudia zisitishwe mara moja. Huku wakitoa nara kama vile 'Mauti kwa Marekani', 'Mauti kwa Aal Saud' na 'Mauti kwa Utawala wa Kizayuni' waandamanaji wametangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wasio na hatia Yemen. Baada ya maandamano hayo kumesomwa taarifa ya kulaani hujuma ya Saudia Yemen na njama za Marekani za kuhakikisha utawala wa Kizayuni unabakia katika eneo. Taarifa hiyo imesema Riyadh, mji mkuu wa Saudia sasa ni mji mkuu wa ugaidi. Halikadhalika wamelaani mpango wa pamoja wa Saudi Arabia na Wazayuni katika kuizingira Yemen na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingizwa nchini humo. Wakati huo huo Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Hilali Nyekundu ya Iran ameashiria hatua ya Saudia kuzuia misaada ya kibinaadmau kutoka Iran isiwafikie wanaohitajia nchini Yemen. Hujatul Islam wal Muslimin Muizz amesema kuwa, meli ya misaada ya kibinadamu kutoka Iran kesho itaelekea Yemen.../mh