Katibu wa mashindano hayo Seyed Mustafa Husseni amesema majaji 12 watakuwa ni kutoka Iran huku wengine 10 wakiwa ni kutoka mataifa mbali mbali duniani.
Ahmed Khalid al-Athamina kutoka Jordan, Seyed Aqil Hussein al-Munawar kutoka Indonesia, Nureddin Mohamedi kutoka Algeria, na Khalil al-Nour bin Muhammad kutoka Malaysia ni kati ya majaji wa kigeni katika mashindano, amesema. Kwa mujibu wa Husseini, mtaalamu maarufu wa Qur’ani kutoka Iran, Sheikh Abdul Rasul Aba indie atakayekuwa mwenyekiti wa jopo hilo.
Awamu ya 32 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yanatazamiwa kuanza katika mji mkuu Tehran mnamo 27 Rajab sawa na Mei 15.
Mashindano hayo yataanza sanjari na mnasaba wa Mab’ath (kubaathiwa au kupewa utume Mtume Muhammad SAW). Mashindano hayo ya kila mwaka yataendelea kwa muda wa wiki moja hadi Ijumaa tarehe 22 Mei.