IQNA

Saudia yaendeleza jinai zake Yemen

14:14 - June 12, 2015
Habari ID: 3313339
Makumi ya watu wameuawa katika mwendelezo wa mashambulizi ya kichokozi ya Saudi Arabia na waitifaki wake nchini Yemen.

Ndege za Saudia zilitekeleza hujuma tofauti katika maeneo ya mkoa wa Sada na mikoa mingine ya Yemen ambapo makumi ya raia wasio na hatia waliuawa na kuharibu miundombinu na kadhalika makazi na taasisi za serikali. Aidha ndege za utawala wa Aal-Saud zilishambulia kituo cha mafuta katika mji wa Razeh mkoani Sada na kupelekea watu wengi kuuawa. Kama hiyo haitoshi ndege hizo ziliushambulia msikiti mmoj katika mji wa Marwan na kuuharibu kabisa. Mashambulizi na jinai kubwa za utawala wa Saudia kwa lengo la kuidhoofisha Harakati ya Kiislamu ya Answarullah ya nchi hiyo na kumrejesha madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abd Rabbuh Mansur Hadi na aliyeamua kujiuzulu madarakani na kukimbilia Riyadh, yalianza hapo tarehe 26 mwezi Machi mwaka huu na hadi sasa yameshindwa kufikia malengo yake. Kwa mujibu wa duru za afya nchini Yemen, zaidi ya watu 4,000 wamekwishapoteza maisha yao wengi wao wakiwa ni raia wasio na hatia. Katika kujibu chokochoko hizo jeshi la Yemen kwa kushirikiana na wanamapambano wa kujitolea, limeshambulia kwa makombora kambi za kijeshi za Malhama na Ainul-Harrah za Saudia na kuangamiza askari kadhaa wa nchi hiyo.../mh

3313331

captcha