Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani katika Taasisi ya Awqaf na Maswala ya Sadaqa nchini Iran amesema maqari hao watashiri katika vikao 500 vya usomaji Qur'ani kote nchini.
Hujjatul Islam Sayyid Mustafa Husseini ameongeza kuwa maustadhi Ahmed Shahat, Adel al-Baz, Faruq Ahmed Zayf, Mahmoud Abdul Basit, Reza Guma Mnasour, na Mahmoud Shahat Anwar ni kati ya maqari wa Misri walioalikwa Iran mwaka huu. Ameongeza kuwa maqari mashuhuri wa Iran pia watashiriki katika vikao hivyo vya Qur'ani. Kila mwaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huandaa vikao vya qiraa ya Qur'ani Tukufu kote nchini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani...mh