Ahmed al-Muslimani alisema makumbusho hayo yatahifadhi picha, hati za maandishi, mikataba, na rekodi za qiraa za maqari wa Misri.
Vitu mbalimbali vinavyohusiana na wasomaji mashuhuri wa Qur'ani wa Misri vitawekwa kwa ajili ya kuonyeshwa katika makumbusho hayo, alieleza.
Aidha, aliongeza kuwa makumbusho hayo yatakuwa chini ya Mtandao wa Redio ya Qur'ani Tukufu, na sehemu maalum na mashuhuri ndani ya jengo la redio na televisheni la Maspero (Mamlaka ya Kitaifa ya Vyombo vya Habari ya Misri) itatengwa kama makao makuu ya makumbusho hayo.
Al-Muslimani amesema kuwa familia za maqari maarufu zaidi tayari zimewasiliana ili kukusanya vitu vyao kwa ajili ya makumbusho hayo mapya.
Baada ya vitu hivyo kupangwa, kuandaliwa, na kuwekwa kwa ajili ya maonyesho, makumbusho hayo yatafunguliwa kwa ziara rasmi.
Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye idadi ya watu takribani milioni 100. Waislamu wanakadiriwa kuwa asilimia 90 ya jumla ya idadi ya watu wa nchi hiyo.
Shughuli za Qur'ani ni za kawaida sana katika nchi hiyo ya Kiarabu, na wengi wa qari bora wa ulimwengu wa Kiislamu, wa zamani na wa sasa, wametoka Misri.
3493283