IQNA

Waislamu Marekani waandamana kulaani kuuawa Wakristo weusi

23:40 - June 22, 2015
Habari ID: 3317492
Waislamu nchini Marekani wamefanya maandamano makubwa kulaani mauaji ya hivi karibuni dhidi ya Wakristo weusi wenye asili ya Afrika ndani ya kanisa moja katika jimbo la Carolina Kusini.

Maadnamano yalifanyika Jumapili chini ya anwani ya "Maandamano ya Umoja kwa ajili ya Amani', na yaliandaliwa na Msikiti wa Jamia wa Charleston kuwaenzi wanawake sita na wanaume watatu waliouawa na mbaguzi wa rangi ndani ya kanisa. Katika maafa hayo kijana mzungu, Dylann Roof mwenye umri wa miaka 21 aliyeathiriwa na mitazamo na fikra za kibaguzi, aliingia katika kanisa la Wamarekani weusi na baada ya kuketi nao kwa muda wa saa moja aliwamiminia risasi na kuua 9 miongoni mwao. Maafisa wa polisi waliokwenda kupekuwa nyumba ya kijana huyo walipata bendera za utawala wa zamani wa ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini na Rhodesia (Zimbabwe ya sasa), suala ambalo ni ishara kuwa kijana huyo ametekeleza mauaji hayo kutokana na chuki za kibaguzi na hamu yake ya kuangamiza watu weusi. Mauaji haya yanaonesha kuwa, chuki za kibaguzi nchini Marekani sasa zimetoka mitaani na kuingia katika awamu ngingine ya kutumia silaha na kumwaga damu.

Uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo mashambulio ya mara kwa mara yanayolenga makanisa ya Wamarekani wenye asili ya Afrika yakiwemo ya kuchomwa moto na kuripuliwa kwa mabomu makanisa hayo.../mh

3317136

captcha