IQNA

Rais Rouhani atuma salamu za Idi ul Fitr

19:08 - July 18, 2015
Habari ID: 3329111
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia ujumbe viongozi wa nchi za Kiislamu akimshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kukamilisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Katika ujumbe huo Rais wa Ira amezipongeza serikali na mataifa ya Waislamu kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idil Fitr.
Rais Rouhani amesema sikukuu ya Idil Fitr ni sikukuu ya kurejea kwenye maumbile safi ya mwanadamu ambayo inamtayarishia kiumbe huyo uwanja mzuri wa kujiepusha na ukatili na misimamo ya kupindukia mipaka. Ameeleza matarajio kuwa, kwa ushirikiano zaidi wa nchi zote za Waislamu, kutashuhudiwa amani, utulivu na usalama endelevu kwa msingi wa masuala ya kiroho, uadilifu na busara kote duniani hususan katika Umma wa Kiislamu.
Rais Hassan Rouhani amemuomba Mwenyezi Mungu awape saada na ufanisi Waislamu kote duniani.
Idil Fitri inaanza kusherehekewa leo hapa nchini Iran baada ya kukamilisha siku 30 za mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.../mh

 

captcha