Ali Larijani ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran alipotembelea maonyesho kuhusu ‘Mapambano ya Yemen’. Larijani ameongeza kuwa mbali na mwamko wa Waislamu kuna nukta zingine pia ambazo zitakuwa na taathira katika mustakabali wa Mashariki ya Kati. Aidha ameonya kuwa madola ya kibeberu yanapanga njama ya kuvuruga zaidi hali ya mambo katika nchi za Kiislamu. Spika wa Bunge la Iran pia ameitaja Yemen kuwa nchi yenye historia ndefu sana katika Mashariki ya Kati na kusema Wayemen ni mashujaa ambao daima wamekuwa na nafasi muhimu katika ushindi wa umma wa Kiislamu.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia kijeshi Yemen tangu tarehe 26 Machi, na hadi sasa watu zaidi ya 4,700 wameshauawa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo.
Saudia imekiuka mapatano ya usitishwaji vita yaliyokuwa yameanza kutekelezwa wiki mbili zilizopita kupitia upatanishi wa Umoja wa Mataifa.
Saudia hata haiuheshimu mwezi mtukufu wa Ramadhani bali iliendeleza mashambulizi yake dhidi ya watu wa Yemen katika mwezi huo mtukufu.