Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Al-Alam, maandamano yamefanyika katika nchi mbali mbali duniani kuanzia Ijumaa kulaani hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya Saudia dhidi ya Sheikh Nimr.
Maandamano yamefanyika katika miji kama vile Sydney, Australia, Auckland, New Zealand, Mexico City nchini Mexico, Sao Paulo, Brazil, Brussels, Belgium, na Paris, Ufaransa.
Sheikh Nimr alitiwa mbaroni mwezi Julai mwaka 2012 kufuatia maandamano ya wananchi katika eneo la Qatif nchini Saudi Arabia.
Anatuhumiwa kuwa alitoa hotuba zilizo dhidi ya utawala wa kifalme na kuwatetea wafungwa wa kisiasa. Kukamatwa Sheikh Nimr kuliibua machafuko makubwa katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Mwezi Machi mwaka huu mahakama ya rufaa ya Saudia iliidhinisha hukumu ya kifo dhidi ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu lakini hukumu hiyo ya kidhalimu bado haijatekelezwa.../mh