Ndege za kivita za Saudia zilitekeleza hujuma za angani katika mkoa wa Hudaydah Alhamisi usiku ambapo idadi kubwa ya raia wameuawa.
Katika kulipiza kisasi uvamizi huo wa Saudia, jeshi la Yemen likishirikiana na wapiganaji wa Ansarullah wamelenga vituo kadhaa vya kijeshi ndani ya Saudi Arabia katika mkoa wa Jizan. Hayo yanajiri wakati Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anayeshughulikia Misaada ya Kibinadamu Stephen O'Brien akitoa wito wa kustitishwa vita Yemen. Amesema mazungumzo, na si silaha, ndio njia muafaka ya kutatua mgogoro wa Yemen.
Saudi Arabia ilianza kuishambulia kijeshi Yemen tarehe 26 Machi mwaka huu kwa lengo la kuiondoa madarakani harakati ya Ansaraullah. Uvamizi huo wa Saudia umepelekea Wayemen wasio na hatia zaidi ya 5,350 kuuawa wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto wadogo. Aidha Saudia imedondosha mabomu katika misikiti, shule, viwanda na mahospitali katika maeneo mbali mbali ya Yemen. Mashambulio hayo ya Saudia yameifanya hali ya kibinadamu nchini Yemen kuwa mbaya mno, huku kukikosekana huduma muhimu za chakula na matibabu.../mh