Kwa mujibu wa gazeti la intaneti la Tishreen tolea la Septemba 13, mashindano hayo yaliwahusisha wanafunzi wa taasizi za kuhifadhi Qur'ani za Al Assad kote nchini Syria.
Duruy a kwanza ya mashindano hayo ilikuwa na washiriki 1,000 waliohifadhi Qur'ani kikamilifu kutoka mikoa ya nchi hiyo ambayo 70 kati yao walifuzu kuingia fainali.
Yasir Ahmad kutoka Halab, Umar Ahmad Hassan Agha kutoka Latakia, na Abdulaziz Tahir Al-Sawas kutoka Halab walichukua nafasi za kwanza katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, Juzuu 20 na Juzuu 10 kwa taratibu.
Muhammad Abdul Sattar Al-Sayyed, Waziri wa Awqaf Syria amesema pamoja na kuwepo matatizo na njama za maadui dhidi ya Syria, nchi hiyo ingali inaongoza katika kuhifadhi Qur'ani. Amesema Syria imeweza kupata hadhi hiyo ya juu kutokana na kuwepo wanazuoni na mahufadh wa Qur'ani Tukufu pamoja na usimamizi wa taasisi za kuhifadhi Qur'ani za Al-Assad kote Syria. Amesema taasisi hizo zilianzishwa na hayati rais wa zamani wa Syria Hafidh al-Assad na zimeendelea kutoa elimu na mafunzo kwa wenye kuhifadhi Qur'ani chini ya uangalizi wa rais wa sasa wa nchi hiyo, Bashar al-Assad amesisitiza umuhimu wa kusambaza elimu ya kuhifadhi Qur'ani.../mh