IQNA

Walemavu wa vita ni picha ya kipindi cha mtihani mkubwa wa taifa la Iran

20:40 - September 20, 2015
Habari ID: 3365553
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei leo Jumapili mjini Tehran kabla ya kuanza Wiki ya Kijihami Kutakatifu hapa nchini amekutana na kufanya mazungumzo kwa karibu na walemavu wa vita na familia zao na kuwajulia hali.

Baada ya kukutana na kuzungumza na walemavu wa vita na familia zao, Ayatullah Khamenei ametoa hotuba fupi akiashiria mashaka na matatizo ya kimwili ya walemavu hao na kusema ujira na malipo yao ni mara dufu na unaozidi kuongezeka kutokana na mtihani huo mgumu. Ameongeza kuwa: Vilema wa vita ni picha ya kipindi cha mtihani mkubwa wa taifa la Iran wakati wa vita vya kujihami kutakatifu na kuwepo vilema hao katika jamii kwa hakika kunabainisha uhakika wa kihistoria, kimaarifa, kisiasa na kimataifa.
Amesisitiza kwamba vilema wa vita kwa upande mmoja wanadhihirisha jinai zilizofanywa na madola yaliyomsaidia Saddam Hussein na katika upande mwingine wanaonesha adhama na utukufu wa hayati Imam Khomeini aliyeweza kulea na kutayarisha watu adhimu kama hawa na kuwatuma katika medani ya vita.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa subira ya wake wa walemavu wa vita na ustahimilivu wao wa mashaka ya kuwahudumia ndiyo kujitolea halisi, jihadi na hamasa. Vilevile amewausia wake, watoto na jamaa wa walemavu wa vita kulinda turathi hiyo kubwa ya kimaanawi na kuichunga.
Kabla ya hotuba hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwakilishi wa Faqihi Mtawala na mkuu wa Taasisi ya Shahid, Hujjatul Islam Walmuslimin Shahidi Mahallati ametoa ripoti kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa walemavu wa vita na familia zao na kusema: Kuwaenzi walemavu wa vita ni kuenzi wanahamasa vigezo waliowafunza wapiganaji wa jihadi njia ya mapambana kwa kukabiliana kwao na mabeberu wa kimataifa.
Vilevile Meja Jenerali Jafari ambaye ni Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sepah ametoa hotuba akiashiria kongamano la pili la kuwaenzi walemavu wa vita na kusema: Watu hao ambao walipata fahari ya kuvaa medali ya ulemavu wa vita kamwe hawakusita kubeba majukumu makubwa ya kulinda Mapinduzi ya Kiislamu na matunda yake na wanaendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhudhuria kwa azma kubwa katika nyanya mbalimbali.../mh

3365284

captcha