IQNA

Indonesia yaikosoa Saudia kwa usimamizi mbovu wa maafa ya Hija

14:32 - September 30, 2015
Habari ID: 3375825
Serikali ya Indonesia imesema siku kadhaa baada ya maafa ya Mina, utawala wa Saudi Arabia umeizuia nchi yake kuwatambua au kutoa msaada wa kitiba kwa raia wake.

Lalu Muhammad Iqbal, afisa mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia amesema Waindonesia 46 walifariki katika maafa ya Mina na kwamba wengine 90 hawajulikani waliko. Kwingineko Pakistan imesema itaanzisha uchunguzi kuhusu maafa ya Mina. Wizara ya Masuala ya Kidini nchini humo imesema Wapakistani 44 walipoteza maisha na wengine 35 kujeruhiwa katika maafa ya Mina.

Alhamisi iliyopita katika ibada ya Hija huko Mina karibu na mji mtakatifu wa Makka, makundi mawili ya mahujaji waliokuwa wakitoka njia mkabala na Mina walikumbana na kusababisha maafa makubwa ambapo watu zaidi ya 4,000 wamethibitishwa kupoteza maisha. Ripoti zinasema kuwa wakuu wa Saudia walifunga njia moja ya kuelekea eneo la Jamarat na kuwalazimisha mahujaji waliokuwa wakielekea huko na wengine waliokuwa wakitoka sehemu hiyo kutumia njia moja. Baadhi ya duru zinadokeza kuwa njia moja ilifungwa ili kumruhusu mtoto wa mfalme wa Saudia kupita na msafara wake uliokuwa na walinzi 350.../

3374620

captcha