IQNA

Watoto 500 wauawa katika hujuma ya Saudia nchini Yemen

17:53 - October 03, 2015
Habari ID: 3377979
Watoto wapatao 505 wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma za ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.

Watoto wapatao 505 wameuawa nchini Yemen kufuatia hujuma za ndege za kivita za Saudi Arabia dhidi ya nchi hiyo masikini zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNCEF, watoto wengine 702 wamejeruhiwa katika uvamizi huo wa Saudi Arabia na waitifaki wake dhidi ya Yemen. UNICEF aidha imesema vijana milioni 1.7 Yemen wanakabiliwa na hatari ya lishe duni huku nchi hiyo ikielekea kutumbukia katika maafa makubwa ya binadamu. UNICEF katika ripoti hiyo ya Ijumaa imesema watoto milioni 1.2 walio chini ya umri wa miaka mitano nchini Yemen wamekumbwa lishe duni. Kwa ujumla ni kuwa karibu watoto na mabarobaro milioni 10 Yemen, ambao ni asilimia 80 ya watu wa nchi hiyo, wanahitajia misaada ya dharura ya  kibinadamu. Saudi Arabia ilianza kuishambulia Yemen tarehe 26 Machi mwaka huu kwa lengo la kuiondoa madarakani harakati ya Ansarullah. Mashambulizi hayo ya Saudia yameua Wayemen wasio na hatia zaidi ya 6,000 wengi wao wakiwa ni raia hasa wanawake, watoto wadogo na wazee. Saudia pia imedondosha mabomu katika misikiti, shule, viwanda na mahospitali katika maeneo mbalimbali ya Yemen.../mh

3377931

captcha