IQNA

Jinai za Israel

UNICEF yalaani Israel kwa kuua watoto zaidi ya 50 Gaza

21:57 - November 04, 2024
Habari ID: 3479701
IQNA - Zaidi ya watoto 50 waliuawa mwishoni mwa juma lililotawaliwa na mashambulizi makali ya utawala haramu wa Israel kaskazini mwa Gaza, na kuwaweka wafanyakazi wa kibinadamu na raia katika hatari kubwa. Hayo ni kulingana na Mfuko wa Dharura wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF).

"Tayari hii imekuwa wikendi mbaya ya mashambulizi kaskazini mwa Gaza," Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell alisema katika taarifa yake Jumamosi. "Katika saa 48 pekee zilizopita, zaidi ya watoto 50 wameripotiwa kuuawa huko Jabalia, ambapo mgomo uliharibu majengo mawili ya makazi yanayohifadhi mamia ya watu."
Huku kukiwa na uhasama unaoendelea, UNICEF iliripoti tukio ambalo gari la mfanyakazi, lililohusika katika kampeni ya chanjo ya polio, lililengwa na utawala wa Israel huko Jabalia al-Nazla.
Inasemekana kuwa ndege isiyo na rubani ya jeshi la Israel  ilifyatulia risasi gari hilo, na kusababisha uharibifu, ingawa mfanyakazi huyo hakuwa amejeruhiwa lakini alishutika sana.
Zaidi ya hayo, shambulizi jingine la Israel ililjeruhi watoto watatu karibu na kliniki ya chanjo huko Sheikh Radwan, ambapo kampeni ya chanjo ya polio inendelea. Russell alitaja matukio hayo yanaonyesha hatari kali zinazowakabili raia katika Gaza na akakazia kuwa sehemu ya “kipindi chenye giza zaidi cha vita hivi vya kutisha.”
 "Mashambulizi haya dhidi ya Jabalia, kliniki ya chanjo, na mfanyakazi wa UNICEF bado ni mifano zaidi ya matokeo mabaya ya mashambulizi ya kiholela dhidi ya  raia katika Ukanda wa Gaza," alisema.
Russell amesisitiza kwamba sheria ya kimataifa ya kibinadamu inaamuru ulinzi wa raia na miundo ya kiraia, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa kibinadamu na maeneo ya makazi.
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakiushambulia Ukanda wa Gaza uliozingirwa tangu Oktoba mwaka jana, baada ya makundi ya muqawama wa Palestina kuanzisha Operesheni ya Mafuriko ya Al-Aqsa katika kukabiliana na miongo kadhaa ya jinai za Israel.
Uvamizi huo wa Israel umewaua zaidi ya Wapalestina 43,340 huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Mashambulizi hayo ya kiholela pia yamesababisha takriban watu milioni 2.3 kuwa wakimbizi wa ndani.

3490559

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel unicef
captcha