IQNA

Rais Putin apitisha sheria ya kulinda vitabu vitakatifu Russia

11:47 - October 17, 2015
Habari ID: 3386346
Rais Vladimir Putin wa Russia ameidhinisha muswada wa bunge la nchi hiyo, Duma, kuhusu kulinda na kuhifadhi heshima vitabu vitukufu vya duni kubwa duniani.

Tovuti ya intaneti ya al Sharq imeripoti kuwa, Siku ya Jumatano Vladimir Putin aliidhinisha muswada kwa kulinda Qur'ani Tukufu, Injili, Taurati na kitabu cha Wabudha. Kwa mujibu wa muswada huo, vitabu hivyo vitakatifu havipaswi kutajwa kuwa ni vitbu vyenye misimamo mikali.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni  mahakama moja huko mjini Yuzhno-Sakhalinsk mji mkuu wa mkoa wa Sakhalin Oblast nchini Russia ilitoa ilitoa hukumu na kudai tafsiri moja ya Qur'ani ni yenye misimamo  jambo ambalo liliibua hasira za Waislamu eneo hilo.
Yaroslav Nilov Mkuu wa Kamati ya Duma ya Taasisi za Umma na Kidini amesema kumchukulia hatua zinazofaa kulinda na kuheshimu vitabu vitakatifu ili visivunjiwe heshima.
Ameongeza kuwa moja kati ya hatua zitakazochukuliwa ni kuitaka Mahakama kuu ya Russia kutoa tangaza la kuwataka majaji kote nchini humo kuzingatia kikamilifu heshima vya vitabu vitakatifu vya kidini na marufuku ya kuvunjia heshima vitabu vitakatifu. Kwa mujibu wa katiba ya Russia, dini rasmi nchini humo ni Ukristo wa Kiorthodox, Uislamu, Uyahudi na Ubudhha.
Kuna Waislamu takribani milioni 20 nchini Russia na wengi wanaishi katika maeneo ya Cucasia, Volga, na eneo la kati mwa nchi hiyo.../mh

3385932

captcha