Wito huo umetolewa na Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu IHRC katika barua kwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad al-Hussein. Katiba barua hiyo, IHRC imetaka utawala wa Saudia ushinikizwe kubatilisha hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr na kumuachilia huru mara moja. Barua hiyo imesmea Sheikh Nimr anashikiliwa kwa tuhuma bandia za ugaidi na kuongoza maandamano dhidi ya utawala. Aidha tume Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu imesema Sheikh Nimr ameteswa sana tokea akamatwe July mwaka 2012 katika eneo la Qatif mashariki mwa Saudi Arabia. Hivi karibuni Mahakama Kuu ya Saudi Arabia ilithibitisha hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr Baqir An-Nimr, mwanazuoni mwandamizi wa Kishia; na hukumu hiyo sasa inasubiri idhini ya saini ya Mfalme wa nchi hiyo kwa ajili ya kutekelezwa. Mwanazuoni huyo amekuwa kila mara akifanya jitihada kubwa za kuwaamsha Waislamu nchini Saudi Arabia, hasa Mashia, ili kupigania haki zao; na hiyo ndiyo sababu ya kukabiliwa na hatua kandamizi za utawala wa Aal Saud.
Tajiriba ya malalamiko na upinzani wa wananchi, tangu Sheikh Nimr alipotiwa nguvuni mwaka 2012 hadi sasa unaonesha kuwa miamala ya kikatili na ya utashi wa kisiasa ya watawala wa Saudia dhidi ya mwanazuoni huyo mwanamapambano anayependwa na watu utakuwa ndio mwanzo wa kudhoofika na hata kusambaratika utawala huo. Kutekelezwa hukumu ya kifo dhidi ya Sheikh Nimr Baqir An-Nimr kutaugeuza utulivu wa wastani uliopo hivi sasa ndani ya Saudia kuwa moto wa tufani ya ghadhabu za wananchi dhidi ya watawala wa ukoo wa Aal Saudi unaoweza hata kufufua majeraha makongwe ya mpasuko na vita vya kuwania madaraka baina yao.