Kila mwaka, waandamanaji hukusanyika nchi ya jengo la ubalozi wa zamani wa Marekani hapa Tehran, ambalo hujulikana kama 'Pango la Ujasusi' ambapo hutoa nara dhidi ya Marekani. Aidha katika miji mikubwa kote Iran waandamanaji hukusanyika katika miji mikubwa kuadhimisha tukio hilo. Novemba 4, ambayo inasadifiana na tarehe 13 ya mwezi Aban katika kalenda ya Kiirani, pia hujulikana kama Siku ya Wanafunzi Iran, kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya Mapambano Dhidi ya Uistkbari. Washiriki hutoa nara na taarifa za kuendeleza mapambano dhidi ya Marekani katika maandamano hayo. Ikumbukwe kuwa miaka 36 iliyopita, kundi la wanafunzi Wairani wa vyuo vikuu waliuteka ubalozi wa Marekani, ambao ulikuwa umegeuka na kuwa kituo kikuu cha ujasusi kwa lengo la kuyaangusha Mapinduzi ya Kiislamu ambayo yalipata ushindi Februari mwaka huo huo wa 1979. Nyaraka za siri zilizopatiakana katika ubalozi huo zilibainisha kuwa kweli kauli ya wanafunzi wanamapinduzi ambao walikuwa wanasema Marekani ilikuwa inatumia ubalozi wake Tehran kupanga njama dhidi ya mfumo changa wa Kiislamu Iran. Katika tukio hilo Wamarekania 52 walishikiliwa mateka kwa siku 444 hadi Januari 20 1981. Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu, Hayati Imam Khomeini alipongeza kutekwa ubalozi huo na kukutaja kuwa ni 'mapinduzi ya pili' yenye umuhimu mkubwa.