IQNA

Watetezi wa Palestina

Waandamanaji New York wanaounga mkono mapambano ya Palestina

21:08 - October 09, 2024
Habari ID: 3479564
IQNA - Katika kuadhimisha kumbukumbu ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyotekelezwa dhidi ya Israel na Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, mwaka jana,  waandamanaji wanaounga mkono Palestina wamejitokeza kwa wingi katika mitaa ya Manhattan, New York, Jumatatu usiku.

Watu kadhaa walikamatwa wakati wa maandamano huko New York yaliyoambatana na maadhimisho ya Oktoba 7, Idara ya Polisi New York, NYPD,ilisema.
Waandamanaji waliandamana katika eneo lote la Lower Manhattan kutoka Wall Street hadi City Hall, Washington Square hadi Union Square na pia waliandamana kupitia Times Square na Grand Central kabla ya kukusanyika Madison Square Park.
Umati mkubwa wa waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina walielekea kwenye bustani ya Union Square Jumatatu jioni na walionekana kuongezeka kwa idadi kabla ya kuelekea kaskazini.
Maandamano hayo yalisitishwa kwa muda katika Bustani ya Bryant kwenye Maktaba ya Umma ya New York kisha yakagawanyika na mengine kuelekea Ukumbi wa Treni ya Moynihan.
Mamia ya waandamanaji kisha walikusanyika katika Bustani ya Madison Square.

3490189

Habari zinazohusiana
captcha