IQNA

UN: Sheikh Salman anashikiliwa kinyume cha sheria

12:53 - November 07, 2015
Habari ID: 3444271
Taasisi moja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imetaka mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain aachiliwe huru kwani anashikiliwa kinyuma cha sheria na utawala wa Aal Khalifa.

Idara ya Umoja wa Mataifa kuhusu vifungo vya kinyume cha sheria imesema Sheikha Salman amefungwa kwa sababu ya uhuru wake wa maoni na kwamba ni kinyume cha sheria kuendelea kumhikilia Sheikh Salman.

Maelfu ya wananchi wa Bahrain kwa mara nyingine tena wamefanya maandamano ya kuukosoa utawala wa Aal-Khalifa sanjari na kushinikiza kuachiwa huru shakhsia wa upinzani nchini humo Sheikh Ali Salman. Maandamano hayo yalifanyika jana baada ya Swala ya Ijumaa katika vijiji vilivyoko na vinavyopakana na mji mkuu Manama, kama vile Diraz, Karzakan, Malkiyah na Bilad al-Qadim. Waandamanaji hao wametaka kuachiwa huru mara moja kwa Sheikh Salman, Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha al-Wifaq, anayezuiliwa na utawala huo tangu Disemba 28 mwaka jana, kwa tuhuma za kujaribu kuupindua utawala wa Aal-Khalifa. Kuendelea kutolewa hukumu za kidhalimu dhidi ya wanaharakati wa kisiasa nchini Bahrain kunajiri katika hali ambayo, makundi ya wapinzani yamekuwa yakisisitiza kwamba, hadi sasa karibu wanaharakati 10,000 wa kisiasa nchini humo wanaendelea kushikiliwa katika jela mbalimbali za nchi hiyo na 150 kati yao wamehukumiwa kifungo cha maisha. Aidha duru za habari zimeripoti kuwa wafungwa 150 ni watoto wadogo.
3443929

captcha