IQNA

Milioni 27 wakiwemo wageni milioni 5 katika Arubaini Karbala, Iraq

19:31 - December 04, 2015
Habari ID: 3459722
Wafanyaziara takribani milioni 27 wakiwemo wageni milioni tano wameshiriki katika maombolezo ya Arubaini ya mjukuu wa Mtume Mtukufu SAW, Imam Hussein AS, katika mji wa Karbala nchini Iraq.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uchukuzu wa Iraq Baqir Jabr al-Zubeidi ambaye ameongeza kuwa  idadi ya wafanya ziara ya Arubaini wamefika milioni 27 katika kilele cha maombolezo hii leo Ijumaa na kwamba asilimia 60 ya walioshiriki katika ibada hiyo ni wanawake. Wafanya ziara kutoka nchi zaidi ya 100 wamekuwa wakimiminika Karbala Iraq kwa muda wa wiki moja sasa pamoja na kuwepo tishio la hujuma za kigaidi kutoka kwa makundi ya Kitakfiri. Aghalabu ya wanaoshiriki katika katika maaadhimisho ya Arubaini ni Waislamu wa madhehebu ya Shia lakini pamoja na hayo mwaka huu idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na hata Wakristo pia wameshiriki katika mjumuiko huo wa kihistoria.
Ikumbukwe kuwa takribani miaka 1376 iliyopita, ilifanyika majlisi ya kwanza ya siku ya Arubaini tangu kuuawa shahidi Imam Hussein AS akiwa na wafuasi wake watiifu wapatao 72 ambao waliuawa shahidi tarehe 10 Muharram mwaka 61 Hijria. Majlisi za siku ya Arubaini hufanyika kila mwaka baada ya kupita siku Arubaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya mjukuu huyo wa  Mtume SAW na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbala.../

3459651

captcha