Siku ya Jumatano watu wawili waliotajwa kuwa wanandoa, waliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa katika kituo cha walemavu huko San Bernardino jimboni California ambapo watu wasiopungua 14 waliuawa na wengine 21 kujeruhiwa. Tukio hilo limetajwa kuwa mbaya zaidi la ufaytuaji risasi hadharani Marekani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Syed Rizwan Farook aliyekuwa na umri wa miaka 28 na mke wake, Tashfeen Malik aliyekluwa na umri wa miaka 27 walidaiwa kutekeleza hujuma hiyo na baadaye wakauawa katika ufatulianaji risasi na polisi. Imearifiwa kuwa wawili hao ni Wamarekani wenye asili ya Pakistan. Kufuatia tukio hilo Waislamu kote Marekani wana hofu kuwa tuhuma kuhusu wawili hao huenda zikapelekea kuenea ubaguzi na chuki zaidi dhidi ya Waislamu. Siku ya Alhamisi Rais Barack Obama wa Marekani alisema kuna uwezekano kuwa ufatuaji risasi huo ni kitendo cha ugaidi. Jumuiya za Waislamu Marekani wamelaani mauaji ya San Bernardino na kutoa wito wa kutolaumiwa Uislamu au Waislamu kutokana na uhalifu unaotnedwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni Waislamu. Huku Marekani ikielekea katika uchaguzi wa rais mwaka 2016, idadi kubwa ya wagombea urais wameonyesha chuki za wazi dhidi ya Waislamu.