Rais Yahya Jammeh amesema kuwa, kwa kuwa raia waliowengi wa nchi hiyo ni Waislamu, Gambia haiwezi kuendelea kuvumilia turathi za kikoloni.
Rais wa Gambia amesisitiza kuwa, wafuasi wa dini nyingine nchini humo hawatabughudhiwa na wanaweza kuishi kulingana na mafundisho ya dini zao.
Rais Jammeh ambaye mwaka 2013 alitangaza kujitoa nchi hiyo katika Jumuiya ya Madola, Commonwealth na kuitaja kuwa ni ukoloni mamboleo, anataraji nchi za Kiarabu zitaisaidia nchi yake ili iweze kuziba pengo la misaada iliyokatwa na itakayokatwa ya madola ya Magharibi. Machi mwaka huu serikali ya Gambia ilibadilisha lugha yake rasmi ya Kiingereza na kuifanya kuwa Kiarabu.
Gambia ni nchi ya magharibi mwa Afrika yenye wakazi milioni moja na laki nane huku asilimia 95 wakiwa ni Waislamu. Gambia ilikoloniwa na Uingereza hadi mwaka 1965 ilipopjinyakulia uhuru.
Nchi hiyo inategemea zaidi kilimo na utalii kama sekta kuu na uti wa mgongo wa uchumi wake.