
Kwa mujibu wa tovuti ya Al Sharq, Mohamed Mokhtar Gomaa Waziri wa Awqaf Misri amesema: "Wizara hii inajitahidi kuwavutia vijana na mabarobaro katika Madrassah za Qur’ani sambamba na kukabuliana na misimamo mikali na wenye kuieneza.”
Sheikh Mokhtar Gomaa ameyasema hayo pembizoni mwa ufunguzi wa msikiti wa Masjidul Hijab katika mkoa wa Aswan nchini Misri na kuongeza kuwa: "Wizara ya Awqaf ya Misri ina mpango ujulikanao kama ‘Madrassah za Kisasa za Qur’ani’ kwa lengo la kuwapa himaya watoto ili wasitumbukie katika misimamo mikali ya kidini.”
Aidha amesema katika kipindi cha wiki mbili zijazo, maimamu wote na waliohitimu katika vyuo vya Qur’ani watashiriki katika mtihani maalumu wa Wizara ya Awqaf kabla ya kupata kibali cha kuanzisha madrassah za Qur’ani.
Sheikh Mokhtar Gomaa amesema Wizara ya Awqaf Misri kudhibiti hotuba zinazozomswa misikitini kwa kutoa vibali tu kwa maimamu waliosoma katika Chuo Kikuu cha Al Azhar na vyuo vilivyo idhinishwa na wizara hiyo na kwa njia hiyo kuzuia hotuba zenye misimamo mikali ya kidini.