IQNA

Vikao 60,000 vya Qur’ani Iran wakati wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi

11:42 - January 20, 2016
Habari ID: 3470068
Shule 60,000 kote Iran zimepanga vikao maalumu vya kusoma Qur’ani Tukufu mwezi ujao kwa mnasaba wa maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa Mohammad Reza Mosayyebzadeh, mkurugenzi mkuu wa masuala ya Qur’ani, Etrat na Sala katika Wizara ya Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu Iran amesema kutakuwa kuwa na maonyesho ya Qur’ani katika shule hizo kwa mnasaba huo.

Ameongeza kuwa, maonyesho hayo yataangazia mafanikio ya Qur’ani na harakati zinazohusiana na Qur’ani za wanafunzi katika shule husika.

Mamilioni ya Wairani mnamo Februari Mosi wataanza maadhimisho ya siku 10 ya kukumbukwa mwaka wa 37 tokea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979, mapinduzi ambayo yalipelekea kuangushwa utawala wa Pahlavi uliokuwa kibaraka wa Marekani.

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na Imam Khomeini RA yalianzisha mfumo mpya ya kisiasa kwa msingi wa mafundisho ya Kiislamu.

3468625

captcha