
Kwa mujibu wa gazeti la Juhaina al Ekhbariya, Kikao hicho cha 11 cha
kila mwaka cha kusoma Qur'ani Tukufu kimehudhuriwa na shakhsia 400 wa kidini na
kijamii, maqarii kutoka Saudi Arabia na nchi jirani za Ghuba ya Uajemi. Kikao
hicho cha kujikurubisha na Qur'ani Tukufu kimefanyika katika Msikiti wa Jamia
ya Ummul Banin katika mji wa Saihat wenye wakaazi wengi Waislamu wa madhehebu
ya Shia.
Kikao hicho cha kimataifa ya Qur'ani Tukufu kimefanyika kwa himaya
ya Taasisi ya Anwar al Qur'an katika mji
huo ulio katika mkoa wa Qatif nchi Saudia.
Kikao hicho cha kujikurubisha na Qur'ani Tukufu kilijumuisha maqarri
maarufu wakiwemo Mohammad Al Busaidi na
Hussein Aal Rabaan kutoka Taasisi ya Anwar al Qur'an ya mjini Saihat, Hashim al
Shaalah, Said Abdulkarim Aal Issa, na Saeed Sharufna ambao ni maqarri kutoka
mkoa wa Qatif, Mohammad Yassin Jubayl ambaye ni qarii kijana wa Kishia kutoka
Bahrain, Ahmad al Muhaysini ambaye ni kati
ya Mashia wa mjini Madina na Haj Hassan Aal Qanbar mmoja kati ya maqarii wa
Kuwait.
Lengo la kuandaliwa kikao hicho cha kujikurubisha na Qur'ani Tukufu
limetajwa kuwa kuimarisha na kueneza mazingira ya Qur'ani katika jamii,
kuwaarifisha maqarii bora na kuimarisha uhusiano baina ya taasisi za Qur'ani
kwa lengo la kustawisha harakati za Qur'ani.
Abdul Jabbir al Shafii Mkuu wa Taasisi ya Qur'ani ya Anwar al Qur'an
alihutubu katika kikao hicho na kusema: "Taasisi hii inajitahidi kuandaa program
ili watu waweze kuvutiwa na mafundisho ya Qur'ani na pia kuwalea vijana na
mabarobaro kwa msingi wa Qur'ani, thamani za kidini na maadili bora.
3469918