
Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo Jumatano mjini wakati huu wa kukaribia maadhimisho ya tukio la Februari 18, 1978 la wananchi wa Tabriz, mbele ya maelfu ya wananchi wa matabaka mbalimbali wa mkoa wa Azerbaijan Mashariki na kusisitiza kuwa, chaguzi mbili za tarehe 26 mwezi huu wa Februari ni dhihirisho la mwamko wa wananchi wa Iran katika kuulinda mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, uhuru na heshima ya taifa lao. Amesisitiza kuwa, kushiriki kwa wingi na kwa mwamko wananchi katika chaguzi hizo kutafelisha tamaa ya maadui wanaotaka wananchi wa Iran wasusie chaguzi hizo.
Chaguzi hizo mbili za Februari 26 ni za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na ule wa
Baraza la Wanavyuoni Wataalamu la kumchagua na kusimamia kazi za
Kiongozi Muadhamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa, adui anafanya njama za kila aina ili afikie malengo yake kupitia uchaguzi, hivyo wananchi wa Iran ambao ndio wamiliki hasa wa nchi hii, wanapaswa kuelewa uhakika wa mambo na kutoruhusu kufanikiwa njama hizo za adui.
Amesema siasa za Marekani na nchi nyingi za Ulaya ziko chini ya ushawishi na ubeberu wa kanali za Kizayuni na kusisitiza kuwa, hata hatua zilizochukuliwa na Wamarekani katika kadhia ya nyuklia, navyo vinapaswa kuangaliwa kwa jicho hilo hilo.
Aidha Ayatulah Khamenei amewashukuru wananchi kwa kujenga hamasa ya kipekee kwenye maandamano ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 11 mwezi huu wa Februari na kuongeza kuwa, jambo hilo linaonesha namna wananchi wa Iran walivyo macho, wasivyotetereka na walivyo na azma ya kweli ya kufanikisha malengo yao matukufu.