
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo limefanyika Alhamisi, Machi 3, katika Mnara wa Milad katika mji mkuu wa Iran, Tehran.
Kati ya walioshiriki katika kongamano hilo ni wasomi na watafiti wa ngazi za juu wa Qur’ani, maulamaa, maafisa wa serikali na taasisi za kiutamaduni, mkuu wa Vyombo vya Mahakama Iran Ayatullah Sadeq Amoli Larijani, mkuu wa mrengo wa Qur’ani katika Majlisi ya Ushauri ya Kislamu, Bunge la Iran, Bi. Laleh Eftekhari, Mkurugenzi wa Idhaa ya Qur’ani Iran Mohammad Hossein Mohammadzadeh na mwenyekiti wa Jumuiya ya Harakati Wasomi Wairani walio katika Harakati za Qur’ani Hamid Saber Farzam.
Akizungumza katika kikao hicho, Bi. Eftekhari amesema kuwepo wanawake 1500 watafiti wa Qur’ani katika kongamano hilo ni ishara ya kustawia harakati za Qur’ani miongoni mwa wanawake nchini Iran.
Naye Sheikh Ahmad Ahmadi, katibu wa kongamano hilo, alisema harakati za Qur’ani za wanawake Wairani hazina kifani duniani. Amebainisha baadhi ya harakati za Qur’ani za wanawake Wairani kuwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya Qur’ani, tafsiri, kuhifadhi na kusoma Qur’ani na pia sanaa zinazohusika na Qur’ani.