IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani nchini Algeria

13:10 - April 23, 2016
Habari ID: 3470265
Awamu ya mwisho ya Mashindano ya Sita ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu yenye anuani ya Taj-ul-Qur'ani yameanza tarehe 21 katika mji mkuu wa chi hiyo, Algiers.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya radioalgerie.dz imeripoti kuwa ufunguzi wa mashindano hayo umehudhuriwa na Muhammad Issa, Waziri wa Awqaf na Masuala ya Kiislamu nchini humo.

Aidha wengine waliohudhuria ni pamoja na Hamid Qarin, Waziri wa Mawasiliano Algeria, Tawfiq Khaladi, Mkurugenzi wa Televisheni ya Kitaifa ya Algeria, Sha’ban Lounakel, Mkurugenzi Mkuu wa Radio ya Kitaifa ya Algeria.

Akihutubu katika kikao hicho, Muhammad Issa ameashiria umuhimu wa taathira za kiutamaduni za Mashindano ya Qur'ani katika jamii na kusema, kutangazwa moja kwa moja mashindano hayo katika radio na televisheni ya kitaifa ni ishara ya kufungamana Waalgeria na dini yao.

Amesema mashindao hayo pia hutoa motisha kwa watu wengi zaidi katika jamii kuhifadhi Qur'ani.

Naye Hamid Qarin amepongeza jitihada za walioandaa mashindano hayo na kusema yatakuwa na taathira chanya. Aidha ametoa wito kwa vyombo vya habari kuakisi kikamilifu mashindano hayo. Awamu ya kwanza ya mashindano hayo yalifanyika Machi 20-30 katika mikoa kadhaa ya Algeria.

Wawakilishi sita wakiwemo wanaume watatu na wanawake watatu wameteuliwa kutoka kila mkoa kushiriki katika mashindano hayo yatakayoendelea kwa takribani wiki moja.

3491005

captcha