Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya alnilin imeandika kuwa kikao hicho kujulikanacho kama 'Darul Masahaf al-Afriqiyah' kinafanyika mjini Khartoum chini ya usimamizi wa Sheikh al-Makashifi na Waziri wa Awqaf wa Sudan na wataalamu kutoka nchi kadhaa za Kiislamu.
Mkutano huo unahudhuriwa pia na wajumbe kutoka Saudia, Qatar, Kuwait, Misri, Uturuki nan chi kadhaa za Afrika.
Mkutano huo utajadili harakati za uchapishaji Qur'ani Tukufu barani Afrika na bajeti ya ya uchapisaji kitabu hicho kitukufu barani Afrika.
Taasisi ya 'Darul Masahaf al-Afriqiyah' ilianzishwa mwaka 1994 kwa lengo la kuhudumia, kuchapisha na kusambaza Qur'ani Tukufu barani Afrika ili kuwafikia mamilioni ya Waislamu bara hilo. Taasisi hiyo yenye makao yake mjini Khartoum ina jopo la wasimamizi 45, wawakilishi wa taasisi za kimataifa na wasomi na wataalamu wa Qur'ani Tukufu.